NEWS

Tuesday 28 May 2024

Chandi afurahishwa na utendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara
Na Mwandishi Wetu, Tarime
---------------------------------------

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (pichani juu kulia) jana Jumanne alitembelea ofisi za Gazeti la Sauti ya Mara mjini Tarime na kueleza kufurahishwa na utendaji wa chambo hicho cha habari.

Katika mazungumzo yake na Wahariri wa Sauti ya Mara, Jacob Mugini (Mhariri Mtendaji pichani chini kulia) na Christopher Gamaina (Mhariri wa Habari hayupo pichani) Chandi alisema gazeti hilo linafanya kazi kubwa ya kutangaza fursa za uwekezaji na maendeleo ya kisekta mkoani Mara.


Mhariri Mtendaji, Jacob Mugini (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti Chandi nakala ya Gazeti la Sauti ya Mara.
--------------------------------------------------

"Mimi niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa weledi ya kutangaza maendeleo ya mkoa wetu, sisi viongozi tutaendelea kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa manufaa ya wana-Mara na Watanzania kwa ujumla," Chandi aliwambia wahariri hao.

Kwa upande wao, wahariri hao walimwahidi kiongozi huyo kuendelea kutangaza maendeleo ya mkoa huo, na wakamdokeza kuwa kwa sasa wanaendelea na maandalizi ya maadhimisho ya miaka mitano ya Gazeti la Sauti ya Mara yanayotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages