NEWS

Sunday 19 May 2024

Jeshi la DRC latangaza kuzuia jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Felix TshisekediRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Bwana Felix Tshisekedi
---------------------------------------------------


Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza kuwa limezuia jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Felix Tshikedi huko Kinshasa lililofanyika jana Jumapili mapema asubuhi.

Msemaji wa jeshi la DR Congo Brig Jenerali Sylavin Ekenge amesema kwenye kituo cha runinga cha taifa RTNC TV kwamba washukiwa kadhaa wanazuiliwa na "hali sasa imedhibitiwa".

Tangazo hili linajiri saa chache baada ya watu wenye silaha kushambulia nyumba ya Vital Kamerhe, mkuu wa zamani wa majeshi na mshirika wa karibu wa Rais Felix Tshisekedi Jumapili asubuhi.

Walioshuhudia wanasema kundi la takriban washambuliaji 20 wakiwa wamevalia sare za jeshi walishambulia makazi hayo na ufyatulianaji wa risasi ukafuatia.

Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zilisema washambuliaji hao walikuwa wanachama wa Vuguvugu la New Zaire linalohusishwa na aliyekuwa mwanasiasa aliyeko uhamishoni Christian Malanga.

Walinzi wawili na mshambuliaji waliuawa katika shambulio la nyumba ya Bw Kamerhe, msemaji wake na ubalozi wa Japan umeandika kwenye machapisho ya mtandao wa kijamii wa X.

 Katika video iliyosambaa mitandaoni , Bw Malanga alisikika akisema kwa Kilingala, lugha ya wenyeji: "Sisi wanajeshi tumechoka, hatuwezi kuandamana pamoja na Vital Kamerhe na Rais FĂ©lix Tshisekedi."

Rais Tshisekedi alichaguliwa tena kwa muhula wa pili katika uchaguzi uliozozaniwa mwaka jana mwezi Disemba.

Alishinda takriban 78% ya kura. Takriban watu 20 waliuawa katika ghasia zinazohusiana na uchaguzi wakati wa maandalizi ya upigaji kura.

Rais Tshisekedi hajatoa tamko lolote kuhusu tukio hili kufikia muda wa machapisho ya habari hii .

Balozi wa Japani katika mji mkuu wa Kongo amewaonya wajapani walioko DRC kutotoka nje.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages