NEWS

Saturday 18 May 2024Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara, Raphael Okello, Afisa Habari wa Mkoa huo, Rainfrida Ngatunga, CEO na Mhariri wa Gazeti la Sauti ya Mara, Jacob Mugini, Naibu Katibu Mtendaji wa MRPC, Asha Shaban na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya MRPC, Malima Lubasha wakijadiliana jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoani humo yaliyofanyika mjini Musoma jana Ijumaa.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Evans Mtambi ambaye pamoja na mambo mengine, aliwahimiza waandishi wa habari kutangaza mambo mazuri ya mkoa huo, ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati inayogharimiwa na Serikali ya Awamu Sita, chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages