NEWS

Sunday 19 May 2024

Mancity yanyakua ubingwa England

Mabingwa wa ligi kuu Uingereza 2023/2024,Manchester City.

--------------------------------------------------

Manchester City Watawazwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza 2023/24 Baada ya Kushinda dhidi ya West Ham katika Siku ya Mwisho ya ligi .

Manchester City waliandika jina lao katika vitabu vya historia vya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuwashinda West Ham United katika siku ya mwisho na kutwaa taji la 2023-24 Jumapili.

‘The Citizens’ kama wanavyojulikana kwa jina la utani,wamekuwa timu ya kwanza kushinda ligi kuu ya Uingereza mara nne mfululizo baada ya kumaliza msimu wakiwa kileleni mwa jedwali mbele ya Arsenal.

Baada ya kuwashinda Tottenham Hotspur katikati ya wiki na kurudi kileleni kutoka kwa Washika mitutu wa London,Maarufu,Arsenal, kikosi cha Pep Guardiola kilikuwa dakika 90 tu kutoka kwenye kuandika historia.

Na walifanya hivyo, wakiongoza kwa mabao mawili bila majibu kupitia Phil Foden, ambaye hapo awali alitawazwa Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu kwa kampeni yake bora.

Muingereza huyo alifunga kutoka karibu na lango ndani ya dakika mbili za kwanza kuvunja ukimya na kuamsha nyimbo za mashabiki wa Etihad.

Kisha aliongeza la pili baada ya Jeremy Doku kumpa pasi Murua katika dakika ya 18.

Nyota wa Manchester City Mwiingereza,Phil Foden (katikati) akishangilia bao lake na wenzake katika Mechi ya Mwisho ya Ligi 

 -------------------------------------------------

Lakini Mohammed Kudus alipunguza pengo kwa bao la kushangaza la akrobatiki ambalo lilitia utata kabla ya mapumziko.

Hata hivyo, Rodri alimaliza wasiwasi kwa kufunga bao la kawaida kutoka pembezoni mwa kisanduku, akihakikisha alama zote tatu na pia taji linalotamaniwa.

Drama iliendelea wakati kiungo wa Czech Tomas Soucek alipotupia kichwa maridadi mwishoni mwa mchezo, lakini Video Assistant Referee ilipoingilia na kukataa bao hilo kwa sababu ya ukiukaji wa sheria ya mpira wa mkono.

Mpaka dakika ya mwisho,Manchester City waliweza kuzoa alama zote tatu na hivyo kulitwaa kombe la ligi kuu Uingereza kwa mara ya nne mfululizo wakiwa na Kocha Mhispania,Pep Guardiola.
 
Chanzo: Sky Sports

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages