NEWS

Tuesday 28 May 2024

Kesi kuhusu jaribio la kumuua rais wa Burundi kwa njia ya uchawi yasikilizwa faraghani



Alain-Guillaume Bunyoni (alizaliwa 23 Aprili 1972) ni mwanasiasa wa Burundi ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Burundi kuanzia tarehe 23 Juni 2020 hadi tarehe 7 Septemba 2022.
--------------------------------------
Katika kesi yake iliyoanza Jumatatu wiki hii Waziri mkuu wa zamani wa Burundi Alain-Guillaume Bunyonyi anakabiliwa na mojawapo ya uhalifu mkubwa ambao ni kujaribu kumuua mkuu wa nchi kwa njia ya uchawi.

Wanaofuatilia kesi hii wanasema uhalifu na mipango ya kupindua serikali ndiyo msingi wa kesi hii, na wanakosoa kuwa kesi hiyo haijaendeshwa wazi.

Bunyoni ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza alishtuhumiwa kwa makosa saba yakiwemo ya kuhatarisha mali ya nchi, ufisadi, kumiliki silaha bila leseni na uhalifu mwingine.

Mnamo mwaka jana, Bunyoni alihukumiwa kifungo cha maisha jela, lakini alikana mashtaka dhidi yake.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages