
Sehemu ya nyuma ya jengo la Zahanati ya Kijiji cha Mangucha iliyojengwa kutokana na fedha zilizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara.
Tarime
-----------
Mageuzi makubwa yameonekana kwenye uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya kwa ajili ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), mkoani Mara.
Nyuma ya mageuzi hayo, kuna uwekezaji wa shilingi bilioni 5.4 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaoendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals..
Ripoti ya hivi karibuni ya mgodi huo, inaonesha umewekeza kiasi hicho cha fedha kuuga juhudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya afya ndani ya halmashauri hiyo.
Fedha hizo zimetumika kugharimia ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na nyumba za watumishi tiba katika maeneo mabalimbali ya halmashauri hiyo.
Aidha, sehemu ya fedha hizo imetumika kununua vifaa tiba ili kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi.
“Tangu mwaka 2020 hadi sasa, Mgodi (North Mara) umewekeza kiasi cha shilingi bilioni 5.4 katika ujenzi wa zahanati, vituo vya afya, nyumba za watumishi na vifaa tiba,” inasema ripoti hiyo.

Muonekano wa sehemu ya majengo ya Kituo cha Afya Genkuru ambacho ujenzi wake pia umechangiwa na fedha kutoka Mgodi wa Barrick North Mara.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa afya ni moja ya sekta zinazopewa kipaumbele na Mgodi wa Barrick North Mara kwa kutengegwa bajeti kubwa chini Mpango Wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Mgodi huo umetumia bilioni 26.86 katika kutekeleza miradi 255 ya maendeleo katika sekta mbalimbali, ikiwemo eimu ya msingi na sekondari, afya, miundombinu ya barabara, maji, miradi ya kiuchumi na mazingira tangu mwaka 2019 ulipokuwa chini ya kampuni ya Barrick.
“Sekta ya afya ni ya pili kwa ukubwa wa uwekezaji wa CSR, ikiwa na asilimia 20 ya fedha zote tulizowekeza hadi sasa,” inafafanua sehemu ya taarifa hiyo.
Uwekezaji huo unaripotiwa kuleta mageuzi makubwa katika kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa halmashauri hiyo, kwa mujibu wa viongozi wa kijamii.
No comments:
Post a Comment