NEWS

Saturday 4 May 2024

Mafuriko Ziwa Victoria: Familia Musoma Vijijini zakimbilia kwenye kituo cha afya
Na Mwandishi Wetu
Mara Online News
---------------------------


Kaya tano katika kisiwa cha Rukuba, Musoma Vijijini zimelazimika kwenda kupata hifadhi kwenye kituo cha afya kisiwani humo baada ya nyumba zao za makazi kuzingirwa na mafuriko ya Ziwa Victoria.

Maji yanaripotiwa kuongezeka katika ziwa hilo, huku makazi ya kaya nyingine zipatazo 32 yakiwa hatarini kuathiriwa na mafuriko hayo.

“Siku ya leo siyo nzuri kisiwani Rukuba katika kata ya Etaro kwani mvua zinaendelea kunyesha na maji katika Ziwa Victoria yanaendelea kuongezeka,” ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini imesema leo Jumamosi.Waathirika wa Kisiwani Rukuba wanasema "maji yamewafuata" kwenye makazi yao kwa umbali wa mita 30 hadi 40.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amewasiliana na ofisi ya Bonde la Ziwa Victoria iliyopo jijini Mwanza na kuambiwa “maji yameongezeka kwa kiasi cha wastani wa kina cha mita 1.65”.

Hivyo, wananchi wanaoishi karibu na ufukwe wa Ziwa Victoria wanahimizwa kufuatilia na kuzingatia utabiri unaotangazwa kila siku na wataalamu wa hali ya hewa kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya mafuriko.

Maji katika Ziwa Victoria lenye kawaida ya ujazo wa maji wa takriban kilomita za ujazo 2,424 (2,424 cubic kilometers) yanaripotiwa kuongezeka kipindi hiki cha mvua.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages