NEWS

Thursday 23 May 2024

Mpanda milima Kirui kutoka Kenya afa akikwea Mlima Everest



Pichani ni mpanda milima maarufu wa Kenya, Cheruiyoti Kirui, aliyeaga dunia akijaribi kufika kwenye kilele cha Mlima Everest.
                            
Mpanda milima maarufu kutoka Kenya aliyetoweka karibu na kilele cha Mlima Everest amepatikana akiwa amekufa.

Joshua Cheruiyot Kirui mwenye umri wa miaka 44 na kiongozi wake wa Kinepali Nawang Sherpa, 44, walitoweka Jumatano iliyopita wakati wakijaribu kufika kilele cha Mlima Everest bila oksijeni ya ziada.

Mwongozaji wake bado hajapatikana na timu ya utafutaji ambayo ilikuwa imetumwa kuwatafuta wawili hao, afisa wa utalii wa ndani aliliambia shirika la habari la AFP.

Kupanda Mlima Everest, kilele cha juu zaidi ulimwenguni, kunachukuliwa kuwa kugumu sana na hatari, hata kwa wapandaji wazoefu.

Cheruiyot alikuwa kwenye misheni ya kuthubutu kufika kilele cha Mlima Everest, bila oksijeni ya ziada.

"Aliandamana na mpanda milima kutoka Nepal, Nawang Sherpa ambaye hatima yake bado haijulikani."

Cheruiyot alikuwa mfanyakazi wa benki na alikuwa amepanda hadi kilele cha Mlima Kenya mara 15.

Kupanda Mlima Everest inahitaji uzoefu mwingi katika kupanda milima mahali pengine, cheti cha afya bora, vifaa na mwongozaji wa Nepal mwenye uzoefu.

Theluji na barafu kwenye mlima husababisha hatari mbaya, kama vile maporomoko ya theluji, na kuna msimu mdogo wa kupanda kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kwa urefu wa mita 8,849, kilele cha Mlima Everest una takriban theluthi moja ya shinikizo la hewa ambalo lipo kwenye usawa wa bahari.

Mlima Everest ndio mrefu zaidi duniani, ukiwa na urefu wa takriban mita 8,848. Uko katika safu ya Himalaya, kwenye mpaka wa Nepal na Tibet Barani Asia.

Kila mwaka, mamia ya watu hujaribu kupanda mlima huu, lakini ni changamoto kubwa sana kutokana na hali mbaya ya hewa na hatari zingine za mazingira. Mlima Everest ulianza kupandwa mwaka 1953 na Edmund Hillary na Tenzing Norgay.

Kilele cha Mlima Everest
uliopo Barani Asia.

Baada ya kupandwa kwa mara ya kwanza mwaka 1953, idadi ya watu wanaopanda Mlima Everest imeongezeka sana. 
 
Kila msimu wa kupanda kuna msongamano mkubwa wa watu wanaotaka kufikia kilele, na hii imeleta changamoto za usalama na mazingira, pamoja na mabaki ya takataka na uchafuzi wa mazingira.

Serikali za Nepal na China (ambayo inadhibiti upande wa Tibet) zimechukua hatua za kudhibiti idadi ya watu wanaopanda kila mwaka ili kudumisha usalama na utunzaji wa mazingira ya eneo hilo.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages