Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.
------------------------------------------------------
Na Mwandishi Wetu
Mara Online News, Serengeti
---------------------------------------
---------------------------------------
Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi leo ameanza ziara ya kikazi wilayani Serengeti.
Ziara hiyo ni ya siku mbili, kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia katika chumba chetu cha habari muda mfupi uliopita.
Baada ya kuwasili wilayani humo, Kanali Mtambi amepata fursa ya kuzungumza na wananchi wa kata ya Rigicha kabla ya kuelekea eneo la Nyiberekera kukagua mradi wa maji.
Mwishoni mwa Machi mwaka huu, Kanali Mtambi aliteuliwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, kuchukua nafasi ya Said Mtanda aliyehamishiwa mkoa jirani wa Mwanza.
Tayari, Kanali Mtambi ameshafanya ziara katika wilaya kadhaa za mkoa huo wa mara ikiwemo Tarime.
No comments:
Post a Comment