NEWS

Friday 24 May 2024

Obama amkaribisha kwa furaha Rais wa Kenya




Rais wa Zamani wa Marekani Barack Obama,(Kushoto),akizungumza na Raisi wa Kenya ,William Samoei Ruto,alipomkaribisha 'Blair House' Marekani.
----------------------------------------------------

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alimkaribisha kwa furaha Rais wa nchi ya Kenya katika Blair House huko Washington, D.C


Rais William Ruto alikutana na Barack Obama katika Blair House siku ya Alhamisi, Mei 23.Viongozi hao walikumbatiana na kubadilishana salamu kwa Kiswahili.


"Habari," Obama alimsalimu Ruto.
"Mzuri sana," Rais Ruto alijibu kwa furaha na tabasamu usoni mwake. 

 

Rais William Ruto yuko kwenye ziara ya siku nne nchini Marekani inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya Kenya na Marekani. Ruto aliwasili Washington, DC, siku ya Jumatano, Mei 22, baada ya kutumia siku moja ya ziara yake ya kitaifa huko Atlanta. 


Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alimkaribisha kwa furaha Bwana Ruto katika Blair House huko Washington, D.C. Rais William Ruto alikutana na Barack Obama katika Blair House siku ya Alhamisi, Mei 23. 


Obama alitoa shukrani za dhati kwa mapokezi mazuri aliyopokea wakati wa safari zake nchini Kenya mnamo Julai 2015, akiwa madarakani, na tena mnamo Julai 2018, baada ya kustaafu urais. Ruto alikuwa naibu Rais wa Kenya wakati wa ziara za Obama kwa nyakati hizo zote mbili. 


Je, Ruto na Obama walizungumza nini?

Katika taarifa, Rais Ruto alisema mazungumzo yake na Obama yalihusu maendeleo ya kidemokrasia, masuala ya hali ya hewa, na changamoto za amani na usalama barani Afrika. 

 

Ruto aliongeza kuwa walijadili fursa kwa vijana wa Afrika ambao ni wenye nguvu na ubunifu katika teknolojia, uvumbuzi, na elimu ya juu na ya kiufundi.


"Tulibadilishana mawazo kuhusu jinsi Kenya na Afrika zinavyoweza kutumia taasisi na uwezo wa kiteknolojia wa Marekani kuendeleza maslahi yao," sehemu ya taarifa ilisema.


CHANZO:KTN NEWS- KENYA
















No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages