NEWS

Thursday 16 May 2024

Waziri Mkuu wa Slovakia apigwa risasiPichani ni Waziri Mkuu wa Slovakia ,Robert Fico
 --------------------------------------------------------


Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico, anapigania maisha yake hospitalini baada ya kupigwa risasi jana katika mji mdogo kaskazini-mashariki mwa Bratislava.

Jumatano jioni, Waziri wa Ulinzi Robert Kalinak alisema Bwana Fico alikuwa amefanyiwa upasuaji kwa zaidi ya saa tatu na hali ilikuwa "mbaya".

Wanasiasa wa Slovakia, ikiwa ni pamoja na rais, wametaja shambulio hilo kuwa ni ‘shambulizi dhidi ya demokrasia’.

Mshambuliaji anayedaiwa alikamatwa eneo la tukio lakini bado hajatambuliwa rasmi na mamlaka.

Shambulio lilitokea huko Handlova, umbali wa kilomita 180 (maili 112) kutoka mji mkuu Bratislava, wakati Bwana Fico alikuwa akiwasalimia watu mbele ya kituo cha jamii cha kitamaduni ambapo mkutano wa serikali ulikuwa umefanyika.

Picha zilionyesha mtu akionyesha silaha na kurusha risasi mara tano kwa waziri mkuu kabla ya kudhibitiwa na walinzi huku maafisa wengine wa usalama wa Bwana Fico wakimpeleka waziri mkuu ndani ya gari lake.

Alipelekwa kwa helikopta hadi hospitali ya karibu kabla ya kusafirishwa kwenda hospitali nyingine huko Banska Bystrica, mashariki mwa Handlova.

Waziri Mkuu wa Slovakia,RobertFico, aliyepigwa risasi akiwasilishwa hospitalini kwa helikopta kwa ajili ya matibabu.


Baadaye Jumatano, Naibu Waziri Mkuu wa Slovakia, Tomas Taraba, aliiambia kipindi cha Newshour cha BBC kwamba anaamini taratibu za kumshughulikia Bwana Fico katika hospitali zilikuwa nzuri.

"Nadhani mwishowe ataishi," Bwana Taraba alisema, akiongeza: "Kwa sasa hayupo katika hatari ya kufa."


Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Matus Sutaj Estok, alisema Bwana Fico alipigwa risasi kwenye tumbo.

"Taarifa za awali zinaonyesha wazi shambulio hilo ni la kisiasa," aliongeza.

Ripoti zisizothibitishwa za vyombo vya habari vya ndani zilisema mtuhumiwa ni mwandishi wa miaka 71 na mwanaharakati wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages