NEWS

Monday 27 May 2024

Zaidi ya Watu 670 Wazikwa Hai katika Maporomoko ya Ardhi Yanayosababishwa na Mvua Nzito Papua New Guinea.Sehemu ya maporomoko ya ardhi yaliyoua mamia ya watu Papua New Guinea
---------------------------------------------

Papua New Guinea


Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa liliripoti idadi ya vifo vya maporomoko ya ardhi huko Papua New Guinea kuwa 670 wakati juhudi za uokoaji zikiendelea.

Mvua kubwa kote duniani kwenye mabara mbalimbali imeendelea kunyesha, ikileta maafa katika namna tofauti.


Huko Papua New Guinea, mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea ilileta maafa katika saa za mapema za Ijumaa, Mei 24, na kusababisha madhara makubwa, ikizika takriban nyumba 150, na kuathiri idadi ya watu inayozidi 670 katika kijiji cha Yambali.

Licha ya juhudi za kishujaa za kuwaokoa wale waliokwama chini ya kifusi, ardhi inayoporomoka imefanya operesheni za uokoaji kuwa hatari, ikiwapa waokoaji mashujaa hatari kubwa, kulingana na Al Jazeera.

"Kuna takriban nyumba 150 na zaidi zilizozikwa hadi sasa. Watu zaidi ya 670 wanakadiriwa kufariki. Ardhi bado inaporomoka, mawe yanaanguka, udongo unapasuka kutokana na shinikizo linaloendelea kuongezeka na maji ya ardhini yanatiririka hivyo eneo hilo linazua hatari kubwa kwa kila mtu," alisema afisa wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, Serhan Aktoprak.

Chanzo: Al Jazeera.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages