NEWS

Sunday, 16 June 2024

Biashara United washambuliwa Tabora




Na Mwandishi Wetu
----------------------------


Baadhi ya viongozi na mashabiki wa Timu ya Biashara United wamevamiwa na kushambuliwa na kundi la watu wanaodaiwa kuwa mashambiki wa Timu ya Tabora United.

Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa shambulio hilo limetokea mjini Tabora leo asubuhi muda mfupi baada ya Timu ya Biashara Unitedi kuwasili Tabora, ambapo inadawa kuwa viongozi wawili wa timu hiyo waliojeruhiwa na kunyang’anywa vitu mbalimbali hawajulikani walipo.

Mbali na watu kujeruhiwa, gari lililobeba baadhi ya viongozi wa Biashara United limepondwa mawe na kuvunjwa vioo. Chanzo cha shambulio hilo hakijajulikana.

Hayo yametokea huku timu za Biashara United na Tabora United zikitarajiwa kuchuana leo jioni mjini Tabora, katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao wa 2024/2025.

Mara Online News inaendelea na juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, na uongozi wa Biashara United kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages