NEWS

Thursday 13 June 2024

Biashara United yainyuka Tabora United 1-0, kurudiana Jumapili ijayo



Wachezaji wa Biashara United wakifurahia ushindi wao dhidi ya Tabora United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma, mkoani Mara jana Jumatano.
-----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Musoma
---------------------------------------


Timu ya Biashara United imetumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma, mkoani Mara kwa kuinyuka Tabora United bao 1-0.

Mechi hiyo ilichezwa jana Jumatano, ikiwa ni mchuano wa kwanza wa mtoano wa kuwania kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao wa 2024/2025.

Bao hilo la Biashara United lilifungwa na mchezaji Herbert Lukindo kwa mkwaju wa penalti dakika ya lala salama.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora ili kumpata mshindi wa jumla atakayecheza Ligi Kuu msimu ujao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages