NEWS

Thursday 27 June 2024

IMF Yakubali Kusaidia Kenya: Ahadi Baada ya Ghasia za maandamano kupinga Kodi

IMF  

Shirika la Fedha la Duniani (IMF) limesema linafuatilia kwa karibu matukio nchini Kenya, ambapo maafisa wa usalama wametuhumiwa kwa kuwapiga risasi waandamanaji wanaopinga Muswada wa Fedha wa mwaka 2024.

IMF imekuwa ikiitaka nchi hiyo ya Afrika Mashariki kutekeleza mageuzi ya fedha ili kupata ufadhili muhimu.

"Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu matukio ya kusikitisha nchini Kenya katika siku za hivi karibuni. IMF inafuatilia kwa karibu hali ya Kenya,"

Taarifa ya IMF iliyonukuliwa na The Star ilisema. "Lengo letu kuu la kuunga mkono Kenya ni kuisaidia kukabiliana na changamoto za kiuchumi inayoikabili na kuboresha mpango wake wa kiuchumi na ustawi wa watu wake," taarifa hiyo iliongeza kusema.

Kauli hiyo ilijiri saa chache baada ya Rais William Ruto kufuta mpango wa ukusanyaji kodi uliopangwa, baada ya kukabiliana shinikizo kutoka kwa waandamanaji.

CHANZO:BBC


Je, unaona msaada wa IMF kama suluhisho la muda mfupi au la kudumu kwa changamoto za kiuchumi za Kenya?"

Kutoa maoni yako gusa maneno yaliyopo chini ya Habari hii yakisomeka kama:

'SIGN IN WITH GOOGLE'


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages