NEWS

Thursday 20 June 2024

Kenya Kufumba na Kufumbua: Maandamano Yashika Kasi Kabla ya Kura ya Muswada wa Fedha.


Kundi la waandamanaji wakipaza sauti dhidi ya Muswada wa Fedha nchini Kenya.
    -------------
Bunge la Kenya linatarajiwa kupiga kura kuhusu mswada mpya wa fedha bungeni, huku baadhi ya raia wa nchi hiyo wengi wao wakiwa vijana wakiandamana kuupinga.

Maandamano ya kuupinga muswada huo ambayoyalianza Jumanne wiki hii yamesababishwa kukamatwa kwa makumi ya watu katika mji mkuu wa Nairobi wakati wakiandamana kupinga mswada mpya wa fedha.

Licha ya mji mkuu Nairobi maandamano haya yamefanyika katika miji mingine mbali mbali ya nchi hiyo.

Wanasheria na makundi ya haki za binadamu wameishutumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani.

Mapema siku ya Jumanne serikali ya Kenya iliunga mkono kwa sehemu madai ya waandamanaji na kutangaza kufuta baadhi ya kodi ikiwemo kodi ya mkate.

Rais William Ruto anasema fedha zaidi zinastahili kukusanywa kupitia ushuru ili kupunguza deni la taifa la zaidi ya dola bilioni sabini.
 
CHANZO:BBC



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages