NEWS

Thursday 6 June 2024

Maafa ,Majonzi, Machungu Sudan: Takribani Watu 150 Wahofiwa Kufa katika Shambulizi, RSF Yashtumiwa.



Moshi Mkubwa Unaotanda angani baada ya Tukio la mauaji ya mamia Sudan kwenye shambulizi. 
------------------------

Takribani watu 150 wanahofiwa kufariki katika mauaji kwenye kijiji kimoja katikati mwa Sudan, lawama zikielekezwa kwa Kikosi cha Wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF), kundi la wanamgambo wanaopigana na jeshi.

Wapinzani hao wamekuwa wakipigania udhibiti wa nchi kwa zaidi ya miezi 13.

RSF haijazungumzia shutuma hizo, lakini siku ya Alhamisi ilijigamba kushambulia maeneo mawili ya kijeshi.

Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii baada ya uvamizi huo wa Jumatano zilionesha maiti kadhaa zikiwa zimefunikwa kwa sanda nyeupe tayari kwa mazishi huko Wad al-Nourah katika jimbo la Gezira.

Video hiyo ilirekodiwa na wanaharakati kutoka kamati ya upinzani ya kitongoji, sehemu ya mtandao wa makundi ya wenyeji kote nchini ambayo yanaunga mkono kurejea kwa utawala wa kiraia.

Kamati ya Upinzani ya Madani ilisema sasa "inasubiri idadi iliyothibitishwa ya waliokufa na waliojeruhiwa".

Mazingira ya mauaji hayo bado hayajulikani, inadaiwa kijiji hicho kilishambuliwa mara mbili na wapiganaji wa RSF siku ya Jumatano.

Hafiz Mohamad, kutoka kundi linaloongoza la kutetea haki za binadamu la Justice Africa Sudan, ameaimbia BBC kwamba watu wengi zaidi bado hawajulikani walipo lakini ilikuwa "vigumu kuwahesabu wote waliofariki" kwa sababu "watu wa RSF bado wako karibu na eneo hilo wakipora".

Serikali ya kijeshi ya Sudan imelaani mashambulizi ya kimataifa ya Wad al-Nourah. RSF ilichukua udhibiti wa jimbo la Gezira, kusini mwa mji mkuu, Khartoum, mwezi Desemba na imekuwa ikishutumiwa kutekeleza dhuluma nyingi dhidi ya raia huko, ambayo inakanusha.

Wakati huo huo, vita vikali vinaendelea kati ya RSF na wanajeshi huko El Fasher, jiji la Darfur magharibi mwa nchi. Kote nchini, zaidi ya watu 15,000 wanakadiriwa kuuawa tangu mzozo huo uanze Aprili 2023.

Je, jamii ya kimataifa ina wajibu gani kuhakikisha kwamba wale waliohusika na mauaji haya wanawajibishwa kikamilifu?

Kutoa maoni yako gusa maneno yaliyopo chini ya Habari hii yakisomeka kama:

' SIGN IN WITH GOOGLE'

CHANZO:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages