NEWS

Sunday 16 June 2024

Mmoja afariki dunia, 17 wajeruhiwa wakitoka fainali ya Waitara Cup Tarime Vijijini



Gari lililopata ajali hiyo
-------------------------------


Na Mwandishi Wetu, Tarime
-------------------------------------


Gari lililokuwa limebeba wachezaji na mashabiki wa timu ya Sirari FC limepata ajali na kusababisha kifo cha mmoja na wengine 17 kujeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni katika njia panda ya Itiryo na Kangariani, wakati wachezaji na mashabiki hao wakitoka kwenye fainali ya mashindano ya Kombe la Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara - yanayofahamika kama ‘Waitara Cup’.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni katika eneo la msitu wa serikali( kumwika) njia panda ya kwenda Itiryo Kangariani mara baada ya finali za ligi la Waitara CUP kumalizika katika kijiji cha Itiryo.

“Majeruhi walikuwa 18 lakini mmoja alifika hospitali akiwa ameshapoteza maisha,” Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Dkt Joseph Mziba ameimbia Mara Online News kwa njia ya simu leo Jumapili.

Hata hivyo, Dkt Mziba amesema hali za majeruhi wengi zinaendelea vizuri na baadhi yao wameruhusiwa kutoka hospitalini.

“Hadi sasa majeruhi 13 wameruhisiwa na tumebaki na wanne, ambapo mmoja alipelekwa Musoma jana,” amefafanua.

Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.

Diwani wa Kata ya Sirari, Amos Sagara ametoa pole kwa wananchi wa kata hiyo kutokana na ajali hiyo.

“Tumeshiriki ligi, kwa bahati nzuri tumeshinda lakini kwa bahati mbaya watu wetu wamepata ajali na tumempoteza mmoja wa wananchi wetu. Natoa pole kwa familia na ndugu wa marehemu, hili ni jambo la kusikitisha,” amesema Sagara.

Mara Online News inaendelea na juhudi za kumpata Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages