NEWS

Tuesday 11 June 2024

Dkt Nawanda avuliwa Ukuu wa Mkoa wa SimiyuDkt Yahaya Ismail Nawanda
--------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt Yahaya Ismail Nawanda.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu leo Jumanne imesema Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu.

Aidha, Rais Samia amewateua Elias Daniel Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, na Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu - kuchukua nafasi ya Dkt Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Naye George Hillary Herbert ameteuliwa na Rais Samia kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikutaja sababu za Rais Samia kufanya mabadiliko hayo ya viongozi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages