NEWS

Sunday 23 June 2024

DED Misungwi atemwa, Missama kutoka Ikulu achukua nafasi yakeJoseph Constantine Mafuru
-------------------------------------


NA MWANDISHI WETU
---------------------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Joseph Constantine Mafuru.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais - Ikulu jana, ilisema Rais Samia amemteua Addo Missama kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo. Kabla ya uteuzi huo, Missama alikuwa Afisa Mwandamizi Ofisi ya Rais - Ikulu.

Rais Samia pia amemteua Hassan Juma Mnyika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, akichukua nafasi ya Lain Ephraim Kamendu ambaye amestaafu. Kabla ya uteuzi huo, Mnyika naye alikuwa Afisa Mwandamizi Ofisi ya Rais – Ikulu.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amemteua Dkt Ashura Abdul Katunzi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), akichukua nafasi ya Dkt Athuman Yusuf Ngenya ambaye amemaliza muda wake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages