NEWS

Wednesday 5 June 2024

RC Mara kuzindua mashindano ya nyama choma Kiabakari kesho



Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.
-----------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Mara
-----------------------------------


Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano ya kuchoma nyama utakaofanyika kimkoa Kiabakari wilayani Butiama kesho Juni 6, 2024.

Mashindano hayo ni sehemu ya mambo ambayo Kanali Mtambi amebuni kwa ajili ya kusaidia kusisimua na kuharakisha maendeleo ya kuchumi kwa wananchi wa mkoa huo.

“Tutaanzisha mashindano mbalimbali, na hayatakuwa mashindano tu, bali yatakuwa yanaamsha shughuli nyingine kwenye jamii,” alisema Kanali Mtambi wilayani Butiama wiki iliyopita.

Alikuwa akizungumza na wakazi wa Kiabakari kuwaeleza jinsi ofisi yake ilivyojipanga kuchangamsha maendeleo ya mkoa huo ambao umejaaliwa na maliasili lukuki, ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya Taifa Serengeti na Ziwa Victoria.

Kanali Mtambi aliwaalika wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ya nyama choma.

“Nawaalika mje, na atakayechoma nyama nzuri ataondoka na zawadi, na mimi pia nitakuja,” alisema.

Hivi karibuni, Kanali Mtambi alisema mbali na kuwa na Hifadhi ya Taifa Serengeti ambayo ni bora barani Afrika, majimbo ya dhahabu kila kona na Ziwa Victoria, pia nyama chama bora inapatikana mkoani Mara.

“Utangazeni mkoa wa Mara vizuri, una mazuri mengi sana, mfano sehemu kubwa ya Hifadhi ya Taifa Serengeti iko katika mkoa wa Mara. Ukija kwenye ufugaji ng’ombe ni safi, hakuna sehemu niliyowahi kula nyama choma super kama Mara.” Kanali Mtambi aliwambia waadishi wa habari wa mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages