NEWS

Thursday 13 June 2024

Rekodi Mpya: Idadi ya Wakimbizi wa kivita na ghasia Duniani Yafikia Kilele Kipya,rekodi za awali zavunjwa!


Watu Wanaosafiri Safari isiyokuwa na Uhakika wakisaka Usalama Popote Duniani katika harakati za kukimbia vita katika nchi zao .
----------------------

Watu milioni 120 wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ghasia na mateso na kuweka rekodi mpya - mwaka wa 12 mfululizo idadi hiyo imeongezeka, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi lilisema.

Idadi ya watu waliolazimika kuhama makazi yao duniani sasa ni sawa na ile ya Japan, shirika hilo lilisema.

Migogoro mipya nchini Sudan na Gaza ilichangia kuongezeka, ambayo mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Filippo Grandi aliita "mashtaka mabaya juu ya hali ya dunia".

Alitoa wito kwa serikali kushughulikia chanzo cha tatizo, badala ya kuwaingiza wakimbizi kisiasa na kugeukia masuluhisho ya haraka kama vile kufunga mipaka.

Badala yake, alizitaka nchi kufanya kazi pamoja kwa ajili ya suluhu za kudumu zaidi.

Migogoro mipya na ya zamani iliongeza idadi ya wakimbizi duniani kote kufikia Aprili 2024, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya shirika hilo kuhusu suala hilo.

Nchini Sudan, vita vilivyoanza kati yamajenerali wapinzani mnamo Aprili 2023 vililazimisha zaidi ya watu milioni tisa kuondoka kwa makazi yao.

Huko Gaza, vita kati ya Israel na Hamas vimesababisha takriban 75% ya wakazi - watu milioni 1.7 - tangu Oktoba.

Mgogoro mkubwa zaidi wa uhamaji wa watu duniani umesalia nchini Syria, ambapo mzozo ulioanza mwaka 2011 unawazuia karibu watu milioni 14 kutoka makwao.

Mamilioni ya watu zaidi walifukuzwa kutoka makwao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Myanmar kwa sababu ya mapigano mwaka jana.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limesema si kweli kwamba wakimbizi wote na wahamiaji wengine walikwenda katika nchi tajiri, likieleza kuwa idadi kubwa ya wakimbizi hao wako katika nchi jirani na zenye kipato cha chini na cha kati.

Idadi ya watu waliokimbia makazi duniani kote imeongezeka karibu mara tatu tangu 2012 na huenda ikaongezeka, Bw Grandi alisema. 
 
Mjadala uko wazi! Je, unafikiri jamii za kimataifa zinapaswa kuchukua hatua gani zaidi kukabiliana na ongezeko la Wakimbizi wa kivita Duniani? Tungependa kusikia maoni yako,karibu!
 
Kutoa maoni yako gusa maneno yaliyopo chini ya Habari hii yakisomeka kama:

' SIGN IN WITH GOOGLE' 
 
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages