NEWS

Sunday 30 June 2024

‘Sura ya Ndoto Yangu’ yampaisha Mary Daniel, Shirika la Her Initiative lamteua kuhudhuria mafunzo maalumMARY DANIEL JOSEPH
---------------------------------


Na Mwandishi wa
Mara Online News
----------------------------

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO) la Nyayo Tanzania, Mary Daniel Joseph kupitia mradi wake wa Sura ya Ndoto Yangu, ameteuliwa na Shirika la Her Initiative kuwa miongoni mwa taasisi 20 zitakazohudhuria mafunzo maalum ya kuboresha shughuli zao.

Mary ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara, amesema amepata uteuzi huo kutokana na juhudi zake za kusaidia wanawake na vijana wa kike, ikiwemo kuwajengea uwezo wa kujiamini, kushiriki kwenye masuala ya uongozi na shughuli za kujikwamua kiuchumi.

“Wakati naendelea kutekeleza hii project (mradi), nimechaguliwa na Shirika la Her Initiative la jijini Dar es Salaam kuwa miongoni mwa taasisi 20 zinazofanya vizuri katika utatuzi wa changamoto kwenye jamii.

“Tutapewa elimu ya namna ya kuboresha shughuli zetu na kuandika miradi (proposals). Pia tutakutanishwa na mashirika mbalimbali, na mwisho wa siku taasisi tatu zitapewa pesa ya kutekeleza miradi yao,” amesema Mary katika mazungumzo na Mara Online News leo.

Amesema alianzisha NGO yake ya Nyayo Tanzania mwaka 2021, na kwamba kupitia mradi wa Sura ya Ndoto Yangu, imeshasaidia wanawake 213 na vijana wa kike zaidi ya 500 katika masuala ya ujasiriamali, kupata mikopo na kuweka akiba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages