NEWS

Thursday 27 June 2024

Tarime: DC Surumbu awaalika wananchi Tamasha la Nyama Choma, RC Mtambi kuwa mgeni rasmiMkuu wa Wilaya ya Tarime, 
Kanali Maulid Surumbu. 
(Picha na Mara Online News)
------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News
------------------------------

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Maulid Surumbu anawaalika wananchi wote wa wilayani humo kuhudhuria na kushiriki Tamasha la Kuchoma Nyama katika viwanja vya mnada wa Mtana.

Tamasha hilo ambalo kwa lugha ya kigeni limeitwa Tarime Nyama Choma Festival, litaambatana na mashindano ya kuchoma nyama.

Taarifa iliyotufikia hivi punde kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, inaeleza kuwa tamasha hilo litafanyika Jumatano ijayo [Julai 3, 2024] kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 10 jioni.

“Dhima ya tamasha hilo ni kutangaza fursa [za biashara] zilizopo, ikiwepo nyama laini na yenye ubora inayotokana na mifugo ya mkoa wa Mara,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Pia taarifa imeweka wazi kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litakuwa la kwanza kufanyika wilayani Tarime, anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages