NEWS

Monday 10 June 2024

Waziri Mkuu Majaliwa akutana na Balozi wa Italia anayemaliza muda wakeWaziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhi zawadi kwa Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Marco Lombardi ambaye amemaliza muda wake, walipokutana jijijini Dar es Salaam jana.
---------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
-----------------------------------------------


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Marco Lombardi ambaye amemaliza muda wake.

Walikutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Es Salaam jana.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu alisema Tanzania itaendelea kuwa mshirika muhimu na wa kimkakati wa nchi ya Italia.

Kwa upande wake Balozi Lombardi alisema licha ya kumaliza muda wake kama Balozi wa Italia nchini Tanzania, bado ataendelea kuisemea Tanzania na kuwa mhamasishaji wa fursa zilizopo nchini hapa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages