NEWS

Thursday 4 July 2024

Biden Asisitiza: Sitajiuzulu, Licha ya Kushinikizwa Kutowania Urais.

Raisi wa Marekani,81, Bw Joe Biden.

Rais wa Marekani Joe Biden alifanya kazi ya kuwatuliza Wanademocratic na wafanyakazi wakuu kwenye kampeni yake siku ya Jumatano, kwani ripoti zilidokeza kwamba alikuwa akiangazia mustakabali wake baada ya mjadala wake mbaya na Donald Trump wiki iliyopita.

Bw Biden alikula chakula cha mchana kwa faragha na Makamu wa Rais Kamala Harris katika Ikulu ya White House huku uvumi ukiongezeka iwapo angechukua nafasi yake kama mgombeaji wa chama katika uchaguzi wa Novemba.

Wawili hao kisha walijiunga na kampeni ya Democratic ambapo Bw Biden aliweka wazi kuwa atasalia kwenye kinyang'anyiro hicho na Bi Harris akasisitiza kumuunga mkono. "Mimi ndiye mteule wa Chama cha Democratic. Hakuna mtu wa kuniondoa. Siondoki," alisema, chanzo kiliambia BBC News.

Maneno hayo hayo yalirudiwa katika barua pepe ya kuchangisha pesa iliyotumwa saa chache baadaye na kampeni ya Biden-Harris. "Wacha niseme haya kwa uwazi na kwa urahisi niwezavyo: Ninagombea," Bw Biden alisema katika barua pepe hiyo, na kuongeza kuwa "alikuwa kwenye kinyang'anyiro hicho hadi mwisho".

Maswali yamekuwa yakiibuka iwapo mzee huyo mwenye umri wa miaka 81 ataendelea na kampeni yake kufuatia mjadala na Trump, ambao ulikuwa na ubabaikaji mkubwa, sauti dhaifu na baadhi ya majibu ambayo yalikuwa magumu kufuatilia. Hilo lilizua wasiwasi katika chama cha Democratic kuhusu uwezo wake kushinda uchaguzi huo.

Shinikizo la kumtaka Bw Biden kujiuzulu limeongezeka siku chache tu kwa saabu kura nyingi zinaonyesha kuwa mpinzani wake wa chama cha Republican anazidi kupata umaarufu. Kura ya maoni ya New York Times iliyofanywa baada ya mjadala huo, ambayo ilichapishwa Jumatano, ilionyesha kuwa Trump alikuwa akishikilia uongozi kwa mbali zaidi akiwa na alama sita.

Na kura ya maoni tofauti iliyochapishwa na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News ilionyesha kuwa Trump ana pointi tatu mbele ya Biden katika majimbo muhimu. Kura hiyo pia ilionyesha kuwa rais huyo wa zamani alikuwa anaongoza kitaifa.

CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages