NEWS

Tuesday, 20 January 2026

Mbunge Mgore asikitishwa na wizi wa gari la kubeba wagonjwa Manispaa ya Musoma

Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Mgore Miraji Kigera.
Na Godfrey Marwa

Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Mgore Miraji Kigera, ameeleza kusikitishwa na tukio la wizi wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) la Halmashauri ya Manispaa ya Musoma likiwa limepakiwa katika ofisi ya Mkurugenzi.

"Kwa bahati mbaya sana sisi Musoma Mjini, Oktoba 10, 2005 gari liliweza kuibwa likiwa Manispaa ya Musoma katika ofisi ya Mkurugenzi. Walioiba sio wananchi, ni jambo lipo linafatiliwa,” Mgore alisema mjini Musoma jana, wakati wa mapokezi ya ambulance nyingine kutoka Wizara ya Afya.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, alisema tayari vyombo vimeanza uchunguzi ili kukomesha mtandao wa wizi huo.

"Katika haya niwambie, yeyote yule atakayeshiriki, atakayeingia kwenye huu mtandao tutambaini tutamkamata na tutamshughulikia. Tunataka tutoe mfano kwa yule aliyeshirikiana na ule mtandao,” alisema Chikoka na kuongeza:

"Makoko pale walipitapita wakataka kutupa doa kwenye mashine, tukaikamata ni hao hao… siku ambayo wanakwenda mahakamani niwahakikishie hatutaenda kimya kimya, hatutaenda gizani, jamii na ulimwengu utajua kwamba huyu ndiyo mtandao, ndiyo mwizi aliyetaka kuwarudisha nyuma wana-Musoma.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages