NEWS

Wednesday 3 July 2024

Mwenyekiti mpya MRPC Jacob akabidhiwa ofisi, Katibu Mtendaji amwahidi ushirikianoMwenyekiti mpya wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob (katikati) akikabidhiwa rasmi ofisi na nyaraka za klabu hiyo kutoka kwa Makamu wake, Raphael Olello mjini Musoma leo Julai 3, 2024. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa klabu hiyo, Pendo Mwakyembe. (Picha na Mara Online News)
------------------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Musoma
--------------------------------------

Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob amekabidhiwa rasmi ofisi ya klabu hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa MRPC, Raphael Okello amemkabidhi Jacob ofisi na nyaraka husika, mbele ya Katibu Mtendaji, Pendo Mwakyembe na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya klabu hiyo mjini Musoma, leo Julai 3, 2024.

Mwenyekiti Jacob akisaini nyaraka mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi ya MRPC leo.
----------------------------------------------

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi, Mwenyekiti Jacob pamoja na mambo mengine, amewaomba wasaidizi wake hao kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya kuistawisha MRPC.

Naye Katibu Mtendaji wa MRPC, Mwakyembe, amemwahidi Mwenyekiti Jacob ushirikiano wa dhati katika awamu nyingine ya utekelezaji wa majukumu ya klabu hiyo.

"Kipindi kilichopita ulifanya kazi sana, ulikivusha chama, tulipata pongezi kutoka mikoa mbalimbali na UTPC (Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania). Wajumbe wenzangu pamoja na Makamu Mwenyekiti naomba tumpe ushirikiano Mwenyekiti wetu.

"Sote tuna mawazo ambayo tukiyatoa kwa pamoja tunayaboresha kwa sababu tuna amani," amesema Mwakyembe ambaye pia ni Makamu wa Rais wa UTPC.

Baada ya makabidhiano hayo, Mwenyekiti Jacob amefanya kikao chake cha kwanza na Kamati Tendaji, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya MRPC.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages