NEWS

Thursday 4 July 2024

Uingereza: Mamilioni kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu kesho




Mamilioni ya watu wanatazamiwa kupiga kura kesho Alhamisi, katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa Julai 2024 nchini Uingereza tangu mwaka 1945.

Vituo vya kupigia kura vilivyowekwa katika majengo kama vile shule za mitaa na kumbi za jumuiya.

Takriban wapiga kura milioni 46 wanastahiki kuwachagua wabunge 650 katika Bunge la Chini.

Matokeo ya kila eneo, au eneo bunge, yatatangazwa usiku kucha hadi kesho kutwa Ijumaa asubuhi.

Vyama vya siasa vinatazamiwa kushinda zaidi ya nusu ya viti 326 ili kuunda serikali ya walio wengi.

Uchaguzi huo, ulioitishwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak Mei 2024, utafanyika chini ya mipaka ya maeneo bunge mapya, kufuatia tathmini iliyopangwa ili kuzingatia mabadiliko ya idadi ya watu.

Mipaka hiyo mipya, kulingana na takwimu za usajili wa wapigakura, imeifanya Uingereza kuwa na wabunge 10 zaidi, na kufikisha jumla ya viti vyake hadi 543.

Idadi ya viti nchini Wales imepungua kwa viti vinane hadi 32, huku jumla ya viti vya Scotland ikishuka kutoka 59 hadi 57. Ireland ya Kaskazini imesalia sawa na 18.

Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anaweza kupiga kura, mradi tu amesajiliwa na ni raia wa Uingereza, au raia anayehitimu wa Jumuiya ya Madola, au Jamhuri ya Ayalandi. Usajili ulifungwa Juni 18, 2024.

Kufuatia mabadiliko ya kisheria mwaka wa 2022, takriban raia milioni mbili wa Uingereza ambao wamekuwa wakiishi nje ya nchi kwa miaka zaidi ya 15 waliweza kujiandikisha kupiga kura. BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages