NEWS

Monday 8 July 2024

Rais Samia atoa ujumbe maalumu Siku ya Kiswahili DunianiRais Dkt Samia Suluhu Hassan
------------------------------------------


NA MWANDISHI WETU
--------------------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa ujumbe maalumu wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kiswahili mwaka huu, na kutuma wito kwa watu wote kutumia lugha hiyo kujenga na kulinda amani na mshikamano kote duniani.

Akitoa ujumbe huo kwa njia ya televisheni jana Julai 7, 2024, Rais Samia pia alituma rai kwa viongozi na kila anayezungumza Kiswahili kutumia lugha hiyo kufundisha watoto elimu na maadili mema pamoja na kukuza biashara.

“Tunapoadhimisha siku hii muhimu tunatambua mchango mkubwa wa wadau wote wa ndani na nje ya nchi kwa kukikuza na kukieneza Kiswahili ambacho sasa kinatambulika na kutumika kikanda na kimataifa.

“Kiswahili ni fursa ya kufanikisha malengo ya maendeleo ya nchi zetu, bara letu la Afrika na duniani kwa ujumla,” alisema Rais Samia.
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages