NEWS

Monday 8 July 2024

CCM Tarime ‘yaminya’ viongozi wawili wa UWT
NA MWANDISHI WETU, Tarime
----------------------------------------------

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime mkoani Mara, kimewasimamisha na kuwavua nyadhifa makatibu wawili wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa kata za Muriba na Nyamwaga zilizopo jimbo la Tarime Vijijini.

Maamuzi hayo yalifikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Tarime kilichofanyika kwenye ofisi ya chama hicho mjini Tarime jana Jumapili.

Inadaiwa kuwa viongozi hao (majina yapo) wamekumbwa na adhabu hiyo kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.

“Wamevunja katiba na kanuni ya CCM,” mmoja wa wajumbe alilidokeza mara baada ya kikao hicho. “Kikao kilikuwa kigumu,” aliongeza mjumbe huyo bila kufafanua.

Hata hivyo, uongozi wa CCM Wilaya ya Tarime hawakuwa tayari kutoa taarifa ya maamuzi hayo mara baada ya kikao hicho.

“Tutatoa taarifa kesho [akimaanisha leo Jumatatu],” Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Tarime, Marema Sollo alisema kwa kifupi alipoulizwa na Sauti ya Mara kwa njia ya simu.
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages