NEWS

Friday, 20 February 2026

NHIF, Mara Press Club kuimarisha mahusiano



Afisa Uhusiano wa NHIF, Theresia Mallya, akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Jacob Mugini, mjini Musoma mapema leo.

Na Mwandishi Wetu
Musoma
-----------------

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya (NHIF), Theresia Mallya, leo Februari 20, 2026 ametembelea ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) mjini Musoma na kufanya mazunguzo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Jacob Mugini.

Mallya amesema waandishi wa habari ni wadau muhimu wa NHIF na kueleza umuhimu wa
kuendelea kushirikiana kuhamasisha suala la huduma ya afya kwa wote, miongoni mwa mambo mengine.

Kwa upande wake, Mugini amemuahidi Mallya ushirikiano mzuri kwa lengo la kujenga taifa lenye watu wenye afya bora.

“Sisi kama Mara Press Club tutaendelea kushirikiana na kuwa sehemu ya kufanikisha
mipango ya NHIF na serikali," Mugini amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages