NEWS

Monday, 2 September 2024

CCM: Dkt Nchimbi yuko tayari kushiriki midahalo ya kujenga



Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi.
--------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi yuko tayari kushiriki midahalo ya kujenga umoja wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na chama hicho tawala, ilifafanua kuwa kiongozi huyo yuko tayari kushiriki midahalo hiyo kadiri taratibu na ratiba yake ya kazi inavyoruhusu.

Taarifa hiyo ya CCM ilikuwa ikijibu lawama za kutoshiriki kwa Katibu Mkuu huyo kwenye mdahalo ulioandaliwa na kituo kimoja cha televisheni nchini.

“Katibu Mkuu hakushiriki wala hakudharau mdahalo huo, alifanya kila jitihada na mwandaaji wa mdahalo huo… alimjulisha kuwa masuala ya vyombo vya habari yanaratibiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, hivyo awasiliane naye, na akampa namba simu ya mkononi… katika kipindi cha wiki tatu hakufanya mawasiliano au kumtafuta.

“Tumeshangazwa na lawama kwa CCM na kwa Katibu Mkuu wakati (mwandaaji) alijua bayana kwamba alikuwa hajapata uthibitisho wowote wa CCM kushiriki. Kushiriki kwenye mdahalo kunahitaji mashauriano na maafikiano kati ya waandaaji na waalikwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM – Habari, Dennis Joe Msacky.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages