NEWS

Monday, 2 September 2024

Mambo 12 yanayoibeba Bodi ya HAIPPA PLC



Mkurugenzi Mkuu wa HAIPPA PLC, CPA Boniface Thomas Ndengo (kushoto) akiwa na mwakilishi wa mgeni rasmi, Mhandisi Mwita Okayo (kulia) siku ya Mkutano Mkuu wa Pili.
-------------------------------------------

Na Mwandishi Maalumu

Mkutano Mkuu wa Pili wa HAIPPA PLC umefanyika, huku Bodi yake ikijivunia mafanikio ya mambo 12 iliyowezesha katika kampuni hiyo ya umma, kwa kipindi cha miezi 23 pekee.

Kampuni hiyo inajishughulisha na uwekezaji, masoko, mitaji na ubunifu - ikilenga kushiriki uwekezaji wa miradi mikubwa na ya kimkakati nchini. Mkutano Mkuu wake wa pili ulifanyika mjini Musoma, Mara wiki iliyopita.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi ambaye aliwakilishwa na Mhandisi Mwita Okayo, alituma wito wa kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kununua hisa katika kampuni hiyo ili kujikwamua kiuchumi.

Mtambi aliipongeza kampuni hiyo na kuahidi kuwa ofisi yake itaendelea kuiunga mkono katika juhudi za ubunifu na mipango ya kuwezesha wananchi ili kuinua uchumi na kuondoa umaskini katika jamii.

Mafanikio 12 yaliyowezeshwa na Bodi ya HAIPPA PLC ndani ya kipindi cha miezi 23 yalitajwa katika mkutano huo, yakiwemo ya kuanzisha Akademi ya Kwanza ya Uwekezaji Tanzania, ambayo imewezesha kuongezeka kwa idadi ya wanahisa kutoka wanane hadi 127.

Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa hisa zilizonunuliwa kutoka 3,400 hadi 435,000, na yatatu yakiwa ni mtaji wa HAIPPA PLC kuongezeka kutoka shilingi 1,700,000 hadi 273,440,000

Bodi pia inajivunia mafanikio ya kuajiri na kuwafunda vijana 10 ambao sasa wapo tayari kuajriwa kuwa watumishi wa HAIPPA PLC.

Aidha, katika kipindi hicho cha miezi 23, Bodi imeweza kufanya vikao tisa ndani ya robo saba, ikiwa ni sehemu ya kudumisha msingi ya utawala bora.

“Kama sehemu ya uwajibikaji kwa wanahisa wake, Bodi imefanikiwa kuitisha mikutano miwili ya mwaka na mkutano maalum, pia imewezesha hesabu za kampuni kwa mwaka 2023 kukaguliwa na kupata hati safi,” ilielezwa katika mkutano huo.

Lakini pia, Bodi imewezesha wanahisa wake kuongeza hisa zao kwa njia ya gawio la hisa kwa asilimia zaidi ya 100 kwa mwaka, na uanzishwaji wa kampuni mbili; ambazo ni HAIPPA Microfinance Limited na BIG4 Limited zinazomilikiwa na HAIPPA PLC kwa asilimia 100.

Vile vile, Bodi imewezesha HAIPPA PLC kuwa kampuni ya kidigitali iliyoijenga mifumo inayofikia makundi yote ya kijamii wakiwemo wakulima, wanawake, vijana, wanafunzi, watu wenye ulemavu, watumishi, wastaafu na watoto

Pia, Bodi imefanikiwa pia kujenga mtandao wake wa uhusiano na wadau muhimu ikiwemo wizara, mashirika ya kimataifa, taasisi za elimu ya juu, ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri, vyombo vya habari, sekta binafsi na vyama mbalimbali vya kijamii.

Bodi ya HAIPPA PLC pia imefanikiwa kujenga mtandao wake wa utoaji huduma na kuwezesha huduma zake kupatikana nchi nzima kupitia ofisi zake zilizopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Mara, na ofisi ya Kidigitali inayopatikana kupitia simu ya kiganjani kwa kupiga *149*46*23# au kupitia tovuti ya kampuni: www.haippa.net.

“Kwa ujumla mtandao huu umewezesha watu zaidi ya 30,000 kufikiwa na huduma za HAIPPA PLC,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa HAIPPA PLC, CPA Boniface Thomas Ndengo.

Kwa mujibu wa CPA Ndengo, HAIPPA PLC kusajiliwa rasmi Oktoba 27, 2022. “Tulianza na wawekezaji wanane walionunua hisa 3,400 zenye thamani ya shilingi 1,700,000.

“Kufikia Desemba 31, 2023 tulikuwa na wanahisa 127 wenye mtaji wa shilingi 233,335,000, na hadi Agosti 28, 2024 mtaji wao ulikuwa shilingi 273,440,000,” alisema CPA Ndengo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya HAIPPA PLC, Dkt Bonamax Mbasa alisema kampuni hiyo imekuwa suluhisho la ukandamizaji lililokuwa likiwakabili wakulima, wafugaji na wavuvi katika masoko ya bidhaa zao.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages