
Rais Donald Trump
Na Mwandishi Wetu
Donald Trump amerejea tena Ikulu ya White House baada ya kuapishwa rasmi jana Januari 20, 2025 kuwa Rais wa 47 wa Marekani, katika hafla ya kihistoria iliyofanyika kwenye jengo la Bunge (Capitol Hill) mjini Washington.
Hii ni mara ya pili kwa Trump kuingia Ikulu ya White House, Marekani kwa kipindi cha miaka minne - baada ya kumshinda Makamu wa Rais anayemaliza muda wake, Kamala Harris katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 2024.
Trump ambaye aliapishwa pamoja na makamu wake, JD Vance, anachukua nafasi ya Joe Biden aliyemshinda katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2021.

UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024
>>ALAT yakagua miradi Tarime Mji, yataka inayoendelea kujengwa ikamilishwe kwa wakati
>>Donald Trump kuapishwa rasmi leo kuwa Rais wa Marekani kwa mara nyingine
>>Dodoma: Stephen Wasira achaguliwa kwa kishindo kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara
No comments:
Post a Comment