
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (CSEE) kwa mwaka 2024/2025 leo, tarehe 23 Januari 2025, saa tano asubuhi katika ofisi za NECTA jijini Dar es Salaam kupitia Katibu Mtendaji wa NECTA,Dkt. Said Mohamed.
Matokeo hayo yanaonesha kuwa watahiniwa 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo wamefaulu kwa kupata madaraja ya I,II,III na IV.
NECTA imesema ufaulu huo umepanda kwa asilimia 3,hivyo kufikia asilimia 92.37 kutoka asilimia 89.39 mwaka 2023.
Kwingineko,katibu mtendaji wa NECTA Dkt.Said Mohamed amefafanua kuhusiana na wanafunzi 67 waliofutiwa matokeo kwa udanganyifu,huku wanafunzi 5 wakiwa wameandika lugha ya matusi kwenye mtihani huo.
No comments:
Post a Comment