NEWS

Tuesday, 4 February 2025

Rais Samia ataka sheria zisaidie kuimarisha mazingira rafiki ya uwekezaji



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akihutubia Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma jana Februari 3, 2025
-------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametaka utekelezaji wa sheria za Tanzania ulenge katika kuimarisha imani ya wawekezaji kwa kuwepo uwazi, mazingira rafiki na taratibu murua za uwekezaji.

Amesema wawekezaji wanaoelekeza macho yao Tanzania wanataka kuwepo kwa uhakika katika nyanja ya ufanyaji biashara kutokana na sheria ambazo ziko wazi.

Akizungumza jijini Dodoma jana wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Sheria nchini na uzinduzi wa shughuli za mahakama mwaka 2025, Rais Samia alisema utekelezaji wa Dira mpya ya Maendeleo ya Mwaka 2050 utavutia uwekezaji, jambo ambalo linalohitaji kuingia mikatamba mbalimbali na sekta binafsi.

Kwa kuzingatia suala hilo, Rais alitaka sekta zote zinazohusika na Haki Madai kujiandaa katika kutoa huduma za haki.

Alisema katika miaka ijayo, Tanzania inatarajia kushuhudia ongezeko kubwa la shughuli za kibiashara na kiuchumi, hali ambayo itahitaji utoaji wa huduma za haki zinazohusika na biashara hizo.

Kwa msingi huo, Rais Samia aliitaka Mahakama na Mabaraza ya Mashauri ya Kodi kuwa wawekezaji wa shughuli za kiuchumi kwa kutenda haki kwa usawa na kwa wakati.

Rais alimsifu Jaji Mkuu, Prof Ibrahim Juma na mhimili wa Mahakama ya Tanzania kwa maendeleo ya utekelezaji wa huduma za sheria, ikiwemo kuimarisha matumizi ya TEHAMA na msisitizo wa kisera wa Mahakama wa kuimarisha Haki Madai.

Kwa mujibu wa Rais Samia, serikali imepokea ushauri wa Chama cha Wanasheria Tanzania wa kuimarisha ushirikiano katika kampeni ya kutoa elimu ya sheria kwa wananchi.

Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania, ambayo ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa katika Afrika Mashariki, imeshuhudia kuwepo kwa madai makubwa ya kukiukwa kwa sheria na taratibu, mwonekano wa upendeleo na madai ya kuongezwa kwa fedha, jambo amblo limekuwa na mvuto kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa - ambao sasa wanatathmini upya kuaminika na kutokuwa na upendeleo kwa mfumo wa sheria wa Tanzania.

Kiini cha wito wa Rais Samia wa kutaka kuwepo uwazi katika sharia za Tanzania ni kuondoa migogoro ya kisheria ambayo inaonekana kushusha imani ya wawekezaji nchini.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages