
Stephen Masato Wasira
Na Mwandishi Wetu, Bunda
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Masato Wasira amewakumbusha viongozi wa chama hicho tawala jukumu la kusikiliza matatizo ya wananchi na kuhakikisha yanapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
“Lazima tusikie wananchi wanasema nini ili tuiambie serikali tuliyoiweka madarakani itatue matatizo yao,” alisema Wasira katika mkutano na viongozi, wanachama wa CCM na makundi mbalimbali ya wananchi wilayani Bunda, mkoani Mara jana Februari 2, 2025.
Alitumia nafasi hiyo pia kukemea majungu ndani ya chama hicho akitaka utendaji wa viongozi ujikite katika kutatua kero za wananchi, wakiwemo wafanyabiashara, wakulima, wavuvi na wafanyakazi.
“Vikao vyetu [CCM] vizungumze mambo ya watu. Hatuwezi kuendesha nchi bila kusikiliza watu. Na vikao vyetu viache kuzungumza majungu,” Wasira alisisitiza.
No comments:
Post a Comment