Muungano wa makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza usitishaji mapigano wa kibinadamu kuanzia Jumanne.
Katika taarifa, kundi hilo - linalojumuisha waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda - lilitaja "sababu za kibinadamu" za kusitisha mapigano, baada ya kuteka maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.
Umoja wa Mataifa umesema takriban watu 900 wameuawa na wengine 2,880 kujeruhiwa katika mapigano ya hivi majuzi karibu na Goma, mji mkubwa wa mashariki mwa DRC, baada ya kutekwa na waasi.
Mataifa ya G7 na EU yamelaani mashambulio hayo kama ukiukaji wa wazi wa uhuru wa DR Congo.
Muungano wa makundi ya waasi - unaojulikana kama Muungano wa Mto Congo - umeshutumu jeshi la Kongo (Congo River Alliance) - kwa kuua watu wakitumia ndege kupiga mabomu maeneo wanayoshikilia.
Iliongeza kuwa haina nia ya kunyakua eneo lolote zaidi, licha ya kusema vinginevyo wiki iliyopita, na itashikilia misimamo yake.
Katika taarifa, muungano huo ulisema: "Tunasisitiza dhamira yetu ya kulinda na kutetea raia na nafasi zetu."
Mapigano ya kikanda yameshuhudia mamia ya maelfu ya watu wakihama makazi yao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Tangu kuanza kwa 2025, zaidi ya watu 400,000 wamelazimika kutoka kwa makazi yao, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.
Rais wa Rwanda Paul Kagame - ambaye pia ni kamanda mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda - alisema hajui kama wanajeshi wa nchi yake walikuwa nchini DRC
"Kuna mambo mengi sijui. Lakini ukitaka kuniuliza, kuna tatizo nchini Congo linaloihusu Rwanda? Na kwamba Rwanda ingefanya lolote kujilinda? Ningesema 100%," aliiambia CNN siku ya Jumatatu.

Chanzo:BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>CCM kutambulisha wagombea wake wa urais kwa wanachama kesho
>>Mara: Wasira ataka kero za wananchi zitatuliwe, aonya majungu CCM
>>Mkutano Mkuu WAMACU wapitisha ununuzi kiwanda cha chai, RC awapongeza kwa kuitangaza kahawa ya Tarime
>>Tarime Mji wapitisha bajeti ya bilioni 30.851/-, DC Gowele asisitiza usafi Hospitali ya Wilaya
No comments:
Post a Comment