NEWS

Wednesday, 30 April 2025

Barrick yashinda tuzo 10 za OSHA 2025



Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Zuhura Yunus, akikabidhi tuzo kwa wafanyakazi wa kampuni ya Barrick mkoani Singida.
--------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Singida

Barrick Tanzania yenye ubia na serikali kupitia kampuni ya Twiga imenyakua tuzo 10 za kimkakati katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) kwa mwaka 2025 iliyofanyika mjini Singida, ambapo Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu umeshinda tuzo kubwa ya mshindi wa juu wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) na Mgodi wa North Mara kuwa mshiriki bora wa maonesho ya mwaka huu (Overall Best OHS Exhibitor).

Tuzo zingine ambazo Mgodi ya Barrick Bulyanhulu umeshinda ni Usalama katika Kuchimba maeneo hatarishi (Advancing in High-Risk Mining Operation), Utoaji wa maelezo kwa ufasaha kwenye maonesho (Best Narrator) na Tuzo bora ya Ubunifu (Best OHS Innovator award).

Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo hizo.
-----------------------------------

Barrick North Mara walishinda tuzo za Ujumuishaji Wafanyakazi wenye mahitaji maalum katika Maonesho (Inclusion of Workers with Special Needs Award), Usalama katika kuchimba maeneo hatarishi (Advancing in High-Risk Operation), Mshindi wa Jumla kwenye washiriki (Overall best OHS Exhibitor) na mshindi wa tatu kwenye CSR.

Kwa upande wake, Barrick Buzwagi walikuwa washindi wa tatu kwenye taaluma ya Ufundi wa kisayansi (Professional and Technical Scientific award) na tuzo ya uwezeshaji wa maonesho (Special recognition of Outstanding support).

Katika Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu (Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, ambaye alisisitiza umuhimu wa waajiri na wafanyakazi kuzingati sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na serikali kupitia Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ili kumlinda mfanyakazi na uwekezaji na biashara kwa ujumla.

Waziri Ridhiwani Kikwete (katikati kulia), akikabidhi tuzo kwa Mrakibu wa Usalama Mgodi wa Barrick North Mara, Meshack Issack.
--------------------------------------

Naye Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, alitumia nafasi hiyo kuwashukuru washiriki wote, waajiri na wafanyakazi kwa kuendelea kuzingatia kanuni na sheria za afya na usalama mahali pa kazi kama injini ya kuongeza uzalishaji kwenye maeneo yao ya kazi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchini kwa ujumla.

Tuzo za Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.
------------------------------------

Mwakilishi wa Barrick katika hafla hiyo ambaye ni Mrakibu wa Usalama, Mgodi wa North Mara, Meshack Issack, alisema Barrick - Twiga itaendelea kushirikiana na serikali katika kulinda afya za wafanyakazi wake pamoja na kudumisha usalama kama nyenzo ya kuchochea uzalishaji, ufanisi na matumizi ya akili mnemba katika sekta ya madini hapa nchini.

Ushindi wa mwaka huu ni mwendelezo wa ushindi katika maonesho ya OSHA yaliyofanyika katika miaka ya karibuni, ambapo mwaka jana pia kampuni ya Barrick ilishinda tuzo tano, ikiwemo tuzo ya mshindi wa jumla.

Suala la Afya na Usalama ni DNA ya kampuni ya Barrick na imeendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa za kidigitali na akili mnemba kuhakikisha inaimarisha zaidi usalama kwenye maeneo yake ya kazi na inatekeleza program za usalama ya ‘Journey to Zero’ na kufanikisha kutokomeza matukio ya ajali kazini na nje ya kazi kwa wafanyakazi wake.

Mbali na kuwekeza katika usalama, Barrick imeendelea kuchangia pato la Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali, kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii kupitia fedha za CSR zinazotolewa na migodi yake, hususan katika mikoa ya Mara ulipo mgodi wa North Mara na Shinyanga na Geita ulipo mgodi wa Barrick Bulyanhulu, hasa katika sekta za afya, elimu na miundombinu ambayo imebadilisha maisha ya wananchi kuwa bora zaidi.

Pia, kampuni ya Barrick imekuwa kinara wa kutekeleza sera ya maudhui ya ndani (Local content) ambayo inaendelea kuwanufaisha wazawa kwa kufanya kazi na migodi yake.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages