Na Mwandishi Wetu
Ujenzi wa mgodi wa dhahabu wa Nyanza wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, utaanza rasmi kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu, Aprili 28, 2025 na kampuni ya Peresus ya Australia.
Mradi huo mkubwa katika kanda ya Ziwa Victoria utamilikiwa na Kampuni ya Ubia ya Sotta ambapo Kampuni itakuwa na hisa asilimia 84 wakati Serikali ya Tanzania itakuwa na hisa asilimia 16.
Taarifa ya Kampuni ya Perseus imeeleza kuwa kiasi cha shilingi trilioni 1.4, sawa na dola za Marekani milioni 523 (pamoja na dharura), zitawekezwa kwenye ujenzi wa mradi huo kabambe unaotarajiwa kuanza kuzalisha dhahabu robo ya kwanza ya mwaka 2027.
Fedha za ujenzi wa mradi huo zitatolewa na kampuni ya Perseus kupitia mikopo isiyo na riba na kwamba kampuni hiyo imetumia dola milioni dola za Marekani milioni 27.5 kwa maandalizi ya awali ya mradi.
Waziri wa Madini, Amthony Mavunde, amesema kuanza kwa mradi huo wa Nyanzaga ni habari njema katika kuimarisha mchango wa tasnia ya madini kwenye uchumi wa taifa, hasa baada ya Rais Samia kuacha milango wazi kwa wawekezaji kutoka nje.
Amesema kwa wananchi wa Sengerema hiyo ni fursa nzuri kwao baada ya kusubiri kwa muda mrefu kuanza kwa mradi huo ambao licha kutoa ajira utakuza uchumi wao na wa taifa ka ujumla.
Tangu kuingia kwenye uchumi wa soko kuptia sera yake ya uwekezaji, Tanzania imejitahidi kuvutia vitega uchumi kutoka sehemu mbalimbali duniani kwenye sekta muhimu kama vile madini, ujenzi wa viwanda, usafirishaji na kilimo, kwa kutaja sekta chache.
No comments:
Post a Comment