
Shaaban Kissu
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Africa Media Group, Shaaban Kissu, ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 7, 2025 na Katibu wa Rais, Waziri Salum, katika hafla ya chakula cha mchana kati ya Rais Samia na waandishi wa habari walioshiriki Tuzo za Samia Kalamu Awards jijini Dar es Salaam.
Kissu ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, amepokewa taarifa hiyo ya uteuzi wake akiwa mshereheshaji katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment