NEWS

Monday, 12 May 2025

Tume ya Uchaguzi yaanzisha majimbo mapya 8, yabadilisha majina ya majimbo 12

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele

-----------------------------
 
Na Mwandishi Wetu

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi jana ilitangaza kuanzishwa kwa majimbo mapya manane na kubadilisha majina ya majimbo mengine 12 yatakayoshiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Jacobs Mwambegele, aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dodoma kuwa tume yake ilifikia uamuzi huo baada ya kupitia maombi kutoka mikoa mbalimbali nchini.
 
Alisema vigezo vya msingi vinavyozingatiwa katika mgawanyo wa majimbo, kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, ni
idadi ya watu (600,000 na 400,000 kwa majimbo ya mijini na 400,000 kwa majimbo ya vijijini).

Majimbo mapya yaliyotangazwa jana kufuatiwa mgawanyo uliopendekezwa nna mikoa kwa Tume mikoa yao katika mabano ni Kivule na Chamazi (Dar es Salaam), Mtumba (Dodoma), Uyole (Mbeya), Bariadi Mjini (Simiyu), Katoro na Chato Kusini (Geita) na Itwangi (Singida).

Majimbo 12 yaliyobadilishwa majina na majina mapya katika mabano ni Chato (Chato Kaskazini), Nkenge (Missenyi), Mpanda Vijijini (Tangsnxika), Buyungu (Kakonko), Bariadi (Bariadi Vijijini), Tabora Kaskazini (Uyui) na Manyoni Mashariki (Manyoni).

Majimbo mengine ni Singida Kaskazini (Ilongero), Manyoni Magharibi (Itigi), Singida Madhariki (Ikungi) na Handeni Vijijini (Handeni).
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages