NEWS

Tuesday, 13 May 2025

Viongozi TANAPA watakiwa kuthamini mawazo ya wafanyakazi chini yao



Makamishna wapya wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
----------------------------------------------

 
Na Mwandishi Wetu
Viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wametakiwa kuwa wasikivu wa mawazo ya wafanyakazi walio chini yao ili kuleta tija na kufikia malengo ya shirika yaliyokusudiwa.

Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Musa Nassoro Kuji, alisema jana jijini Arusha kwamba kiongozi mzuri ni yule aliyetega masikio yake kusikiliza mawazo ya watu anaowaongoza mahali pake pa kazi.

Kamishna Kuji aliyasema hayo wakati wa hafla ya kuwaapisha Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi tisa ili kuboresha utendaji kazi wa shrike.

“Nendeni mkachape kazi kwa bidii na weledi huku mkiishi viapo vyenu. Kiongozi mzuri ni yule anayesikiliza mawazo ya watu wake,” alisema bosi huyo wa TANAPA.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Simon Aweda, ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi, akizungumza kwa niaba ya wenzake walioapishwa aliishukuru Bodi ya Wadhamini TANAPA na menejimenti ya shirika kwa kutambua juhudi zao na kuwapandisha vyeo.

“Tunaishukuru Bodi ya Wadhjamini na uongozi wa shirika kwa kutuamini na kutukabidhi majukumu haya na tunaahidi kufanya kazi kwa bidii na weledi kufikia malengo ya shirika,” alisema Aweda.

Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi waliopandishwa vyeo jana ni Simon Aweda, Catherine Mbena, Marckyfarreny Rwezaula, Nuhu Masay, Glad Ng’umbi, Dkt Halima Kiwango, Halid Mngofi, Catherine Mwamage, na Julius Rutainurwa.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages