
Jaji George Mcheche Masaju
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Jaji George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo Juni 13, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Jaji Masaju sasa anachukua nafasi ya Prof. Ibrahim Jamis Juma ambaye amestaafu.
No comments:
Post a Comment