NEWS

Friday, 13 June 2025

Mechi ya Dabi ya Kariakoo “Simba na Yanga” yasogezwa Juni 25




Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara imetangaza kusogeza mbele mechi namba 184 ya ligi hiyo kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC iliyopangwa kuchezwa Jumapili Juni 15, 2025 mpaka Juni 25, 2025.

Mvutano juu ya hatima ya mchezo huo ambao umedumu kwa takriban miezi mitatu sasa huenda ukafika tamati kufuatia tarehe hiyo mpya iliyopangwa.

Awali, mechi hiyo iliopangwa kuchezwa Machi 8, 2025 uliahirishwa kutokana na sintofahamu iliyojitokeza usiku wa Machi 7, 2025 kisha ikapangwa kufanyika Machi 15, 2025 ambayo pia imesogezwa mbele kwa siku 10 zaidi mpaka Machi 25, 2025.

Aidha, mapema leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Simba na Yanga Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Read Also Section Example

2 comments:

  1. suluhisho ni muhimu kwa mechi zetu kwani mataifa wengine wanatutazama hivyo ni muhimu tusipoiteze mtamo wetu😒😒😒

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages