NEWS

Thursday, 12 June 2025

Mwanasoka nyota wa kimataifa wa zamani Ibrahimovic azuru Hifadhi ya Taifa Serengeti



Zlatan Ibrahimovic akifurahia mandhari ya Hifadhi ya Taifa Serengeti eneo la Kogatende jana.
-------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Nyota wa zamani wa klabu za soka za Ajax, PSG, AC Milan, Barcelona na Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, ambaye kwa sasa ni mmoja wa washauri katika uongozi wa mabingwa mara saba wa UEFA, AC Milan, yupo ziarani nchini Tanzania.


Zlatan ambaye pia aliyepata kuiongoza Timu ya Taifa ya Sweeden, jana aliposti kwenye mitandao ya kijamii akiwa eneo la Kogatende lililopo upande wa wilaya ya Tarime katika hifadhi maarufu duniani - Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania, eneo ambalo ni kitovu cha uhamaji wa wanyama maelfu wanaovuka Mto Mara.

Kwa mujibu wa wataalamu, eneo la Kogatende ndipo mwezi Juni wanyamapori wengi, hasa nyumbu hujaa wakiwa tayari kufanya tukio mashuhuri kwa sasa duniani la kuvuka Mto Mara (World’s Biggest Wildebeest Migration).

“Wengi wanakuja na Agosti kuna ‘breaking news’ kubwa kuhusu mastaa na utalii wa Tanzania,” mmoja wa mawakala wakubwa wa utalii nchini amedokeza.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages