NEWS

Monday, 9 September 2024

Rais Samia aagiza uchunguzi wa kina kifo cha kiongozi wa CHADEMA



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ameviagiza vyombo vya usalama nchini kuchunguza na kumpelekea taarifa ya kina kuhusu kifo cha Mjumbe wa Sekretarieti ya chama cha upinzani - CHADEMA Taifa, Ali Mohamed Kibao.

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

“Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka.

“Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii,” Rais Samia aliandika kwenye ukurasa wake wa X jana.

Jeshi la Polisi Tanzania lilithibitisha kifo cha Kibao ambaye anadaiwa kutekwa na watu ambao hawajafahamika siku moja kabla ya mwili wake kuokotwa juzi ukiwa utelekezwa eneo la Ununio, Tegeta jijini Dar es Salaam.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages