![]() |
| Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman |
Na Mwandishi Wetu
Tume ya Uchunguzi wa matukio ya vurugu
zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025 imeanisha mambo
sita yatakayochunguzwa.
Mwenyekiti
wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, ameeleza katika taarifa
yake kwa vyombo vya habari leo Desemba 1, 2025 kwamba eneo moja
litakalochunguzwa ni kubaini chanzo halisi cha matukio hayo.
Amesema
jambo jingine litakuwa kuchunguza lengo lililokusudiwa na watu ambao tume
itaona walipanga kutekeleza vitendo hivyo.
Tume
hiyo pia itabainisha madhara yaliyojitokeza ikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu
wa mali na madhara ya uchumi na kijamii.
Tume
hiyo pia itachunguza mazingira na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serkali
na vyombo vyake na mtu mwingine yeyote.
Katika
kukamilisha kazi, Jaji Mkuu Mstaafu Othman amesema tume yake itatoa mapendekezo
ya maeneo yanayohitaji kuimarishwa ili kuongeza uwajibikaji kwa viongozi na
raia katika kudumisha amani, utawala bora, haki za binadamu, utawala wa sheria
hadi kufikia maridhiano kitaifa.
Mwishowe,
tume hiyo itachunguza jambo lolote ambalo itaona linaendana na majukumu yake.

No comments:
Post a Comment