NEWS

Monday, 22 June 2026

Barrick North Mara wapeleka misaada kwa familia 60 kwenye vijiji jirani, Gereza la Tarime



Wafanyakazi wanawake kutoka Barrick North Mara wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya familia 60 walizozipatia misaada mbalimbali ikiwemo majiko ya gesi safi ya kupikia jana.

Na Mwandishi Wetu
Tarime
-------------

Wafanyakazi wanawake wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara pamoja na wanaotoka kwenye kampuni za wakandarasi wa mgodi huo wamepeleka misaada mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu katika Gereza la Tarime, mkoani Mara.

Wafanyakazi hao kutoka mgodi huo unaoendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na kampuni ya Twiga Minerals, walikabidhi misada hiyo jana Jumamosi.

Misaada hiyo ambayo imenufaisha kila mfungwa na mahabusu wa kike katika gereza hilo ni magodoro 25, blanketi 25, taulo za kuogea 25, vitenge pea 50, sabuni za kuogea katoni 25, ndala pea 25, dawa za meno pakti 48, sabuni za kufulia mifuko mitano na taulo za kike 372.

Orodha ya misaada hiyo pia ilihusisha unga wa mahindi kilo 300, maharage kilo 100, mchele kilo 50, chumvi pakti 63 na mabati 50.

Aidha, wafanyakazi wanawake walimpatia mfungwa mwenye mtoto wa umri wa miezi 11 gerezani hapo misaada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nguo za mtoto pea 13, viatu vya mtoto pea mbili, sweta pea tatu,, sabuni 12 za kuogea za mtoto, pampers boksi 10 na mafuta ya kujipaka.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, ambaye aliwashukuru wafanyakazi hao wa Barrick North Mara kwa moyo wa upendo, huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo kutoka Barrick.

Mkuu wa Wilaya, Meja Edward Gowele (aliyevaa shati la bluu), viongozi wa Gereza la Tarime na wafanyakazi wanawake kutoka Barrick North Mara wakiwa katika hafla ya kukabidhi misaada hiyo.

Mbali na kupeleka misaada hiyo katika Gereza la Tarime, wafanyakazi wanwake hao kutoka Barrick North Mara walipeleka misaada mingine kwa familia 60 katika jamii ya vijiji vilivo jirani na mgodi huo.

Kila familia ilipata mchele kilo 20, unga kilo 10, mafuta ya kupikia (kula) lita tano, sukari kilo 10, maharage kilo 10, chumvi katoni moja, majani ya chai, mkeka na majiko ya gesi safi ya kupikia.

Wafanyakazi hao walitoa misaada hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake katika sekta ya madini Duniani kwa mwaka huu wa 2026.

Mgodi wa Barrick North Mara na wakandarasi wake wametoa ajira nyingi kwa wanawake, wengi wao wakiwa ni kutoka vijiji vilivyo jirani na mgodi huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages